Wakazi wa vijiji kadhaa vilivyopo katika jimbo la Tete lililopo Kaskazini mwa Msumbiji huenda wakakabiliwa na njaa baada ya mazao yao kuharibiwa na mafuriko na hali mbaya ya hewa.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya Msumbiji imesema kuwa kabla ya Kimbunga Idai pamoja na Kimbunga Kenneth kuyakumba maeneo kadhaa ya nchi hiyo likiwemo jimbo hilo la Tete, maeneo hayo yalikumbwa na ukame ulioathiri takribaini wakulima Elfu Moja wengi wao wakiwa ni wa jimbo hilo.
Kwa sasa wakulima hao wameiomba serikali kuwapatia mbegu kwa ajili ya kuanza shughuli za kilimo katika msimu ujao, kwa kuwa mbegu walizohifadhi zimeharibiwa na mafuriko.