Watumishi wa NAOT watakiwa kuzingatia maadili

0
412

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Umma na Utawala Bora Dkt Francis Micheal amewaasa watumishi Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali (NAOT) kuzingatia maadili wanapotekeleza majukumu yao na kuepuka vitendo viovu vikiwemo vile vya rushwa.

https://www.youtube.com/watch?v=7bFEnylfZd0&feature=youtu.be

Dkt Francis ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi  hiyo ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali na kuwataka kuepuka kasoro katika kazi zao za ukaguzi.