Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi amesema kuwa serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 19 kwa ajili ya kuwalipa wananchi waliochukuliwa maeneo yao na Jeshi.
Akijibu swali Bungeni jijini Dodoma, Dkt Mwinyi amesema kuwa fedha hizo ambazo zilitengwa katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 na zitaendelea kutolipwa mpaka madai hayo yatakapomalizika.
wananchi ambao wanadai kulipwa fidia ya maeneo yao.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu amesema kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kusambaza nishati ya gesi asilia katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo yale ya vijijini.
Bunge linaendelea na vikao vyake jijini Dodoma ambapo Wabunge wanajadili bajeti ya wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.
