Waandamana kupinga kuahirishwa kwa mitihani

0
619

Wanafunzi wa shule za sekondari nchini Somalia wameandamana katika mitaa mbalimbali ya mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu baada ya Wizara ya elimu ya nchi hiyo kuahirisha mitihani ya kitaifa kwa madai kuwa mitihani hiyo imevuja na kuuzwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kuahirishwa kwa mitihani hiyo kumewaathiri Wanafunzi wanaosoma kwenye shule Tisini za sekondari ambazo nazo zimewekwa chini ya ulinzi mkali baada ya kutokea kwa maandamano hayo.

Ili kukabiliana na maandamano hayo, vikosi vya Somalia vimelazimika kutumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kwa lengo la kuwatawanya wanafunzi hao ambao wamekua wakifanya uharibifu wa mali mbalimbali.