Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, – Ayoub Mohamed Mahmouh ameagiza kufungwa kwa baadhi ya biashara katika kipindi hiki cha Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mahmouh amezitaja biashara hizo kuwa ni pamoja na zile za vileo na vyakula katika migahawa isiyo ya kitalii.