Rais John Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maabara mpya ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya – MUST na kukitaka chuo hicho kuendelea kufundisha Sayansi na Teknolojia kwa kuwa viwanda vingi vinavyoanzishwa hivi sasa vinahitaji wataalamu wa aina hiyo.