Rais Magufuli azungumza na Wafanyakazi

0
564

Rais John Magufuli amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Wafanyakazi na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Akizungumza wakati wa sherehe za Wafanyakazi –  Mei Mosi zilizofanyika Kitaifa katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya, Rais Magufuli amewataka Wafanyakazi nchini kufanya kazi kwa bidii, kwani kazi ni msingi wa maendeleo.

 Amesisitiza kuwa, serikali itaendelea kuboresha maslahi ya Wafanyakazi kadri uchumi utakavyoendelea kukua, na kwamba muelekeo unaonyesha mambo yanaendelea vizuri.

Kauli mbiu ya siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa kwa mwaka huu ni Tanzania ya Uchumi wa Kati inawezekana, Wakati wa Mishahara na Maslahi Bora ya Wafanyakazi ni sasa.

Sherehe hizo za Mei Mosi Kitaifa zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo.