Serikali yashauriwa kulipa umuhimu somo la dini

0
442

Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga mkoani Kagera,- Almachius Rweyongeza ameishauri serikali kuufanyia marekebisho mfumo wa elimu ikiwa ni pamoja na kulipa umuhimu somo la dini mashuleni, ili kujenga jamii yenye watumishi wenye hofu ya Mungu, watakaowajibika na kuwatumikia wengine kwa moyo wa uadilifu.

Askofu Rweyongeza ametoa ushauri huo wakati wa Misa ya Pasaka ambayo kitaifa imefanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu George la Jimbo Katoliki la Kayanga wilayani Karagwe.