Jokate ateuliwa Katibu Mkuu UWT

0
155

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imemteua Jokate Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Kabla ya uteuzi huo Jokate alikuwa mkuu wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Pia imemteua Fakii Raphael Lulandala kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa
mkuu wa wilaya ya Momba mkoani Songwe.

Katika hatua nyingine Kamati Kuu imemteua Hamad Khamis Hamad kuwa mgombea wa CCM wa nafasi ya Uwakilishi katika jimbo la Matembwe.