Tatizo sio wawekezaji, ni watendaji wa serikali

0
115

Mbunge wa Msalala Iddi Kassim Iddi, amesema changamoto ya kutofanyiwa kazi kwa miradi mbalimbali ya wawekezaji Serikalini kwa asilimia kubwa inasababishwa na baadhi ya watendaji serikalini na matatizo wanayo wao na sio wawekezaji.

Iddi ambaye pia amemwakilisha Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Nishati na Madini, ameyasema hayo wakati wa ufungaji wa maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.

Ameongeza kuwa, hata baadhi ya changamoto ya barabara mkoani Geita tayari wawekezaji wameshatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo lakini baadhi wa watendaji serikalini ndio wanaokwamisha ujenzi huo.

Ameiomba Serikali kutunga sera ya msamaha wa kodi kwa wachimbaji wadogo na pia kuondoa ukomo kwa makampuni yanayofanya utafiti wa madini ili kuyapa muda wa kufanya utafiti huo zaidi.