Barcelona moto, yatinga nusu fainali

0
312

Timu ya Barcelona imetinga hatua ya Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya kuifunga Manchester United mabao Matatu kwa Bila katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Camp Nou.

Mabao ya Barcelona yamefungwa na Lionel Messi aliyefunga mabao Mawili na Philippe Coutinho.

Katika mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, Juventus imefungwa mabao Mawili kwa Moja na Ajax na kutupwa nje ya michuano hiyo huku Ajax ikitinga hatua ya Nusu fainali.

Mabao ya Ajax yamefungwa na Van De Beek na DE Ligt wakati bao la kufutia machozi la Juventus likifungwa na Cristiano Ronaldo.

Michezo mingine ya Nusu fainali inachezwa  hii leo kwa kuzikutanisha Liverpool na Porto na Manchester City inakutana na Tottenham Hospurs.