HESLB yatoa mafunzo kwa Wanafunzi

0
268

Wanafunzi wa kidato cha Sita kutoka shule mbalimbali za sekondari mkoani Dodoma wameishukuru Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa kuwapatia mafunzo ya namna ya kuomba mikopo pindi wanapomaliza masomo yao.

Wanafunzi hao wametoa ombi hilo jijini Dodoma wakati wa mafunzo hayo ambayo lengo lake ni kuwahamasisha kuomba mikopo endapo watafaulu na kukosa uwezo wa kulipa ada ya elimu ya juu.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mkoa wa Dodoma, – Octavia Selemani amesema kuwa lengo la kutoa mafunzo hayo ni kupunguza usumbufu unaotokana na wanafunzi wengi kushindwa kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa usahihi.