TTCL kuunganisha mataifa ya afrika

0
107

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amelitaka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuhakikisha linaendelea kutoa huduma bora za mawasiliano ili kurahisisha shughuli za maendeleo na kuunganisha mataifa ya Afrika katika masuala ya mawasiliano na mtandao.

Hayo yamebainishwa leo katika hafla ya utiaji saini mkataba wa makubaliano ya kuunganisha mkongo wa taifa wa mawasiliano wa NICTBB na mkongo wa taifa wa mawasiliano unaosimamiwa na ESCOM- Malawi ambao umeshuhudiwa na mawaziri kutoka
wizara zinazohusika na mawasiliano nchini Tanzania na Malawi hafla iliyofanyika mjini Unguja.

Aidha, Waziri Nape amesema mkataba huo ni matunda ya ziara ya Rais Samia Suluhu katika nchi za Afrika ikiwemo ziara yake nchini Malawi iliyozaa mkataba huo wa kibiashara baina ya nchi hizo mbili.