Tanzania kutoa mchango zaidi IFAD

0
102

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Geraldine Mukeshimana Ikulu, Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Makamu wa
Rais amesema Tanzania itaendelea kutoa mchango wake IFAD ili kuwezesha utekelezaji wa miradi inaofanywa na mfuko huo.

Amesema mageuzi katika sekta ya kilimo ni kipaumbele cha Serikali ya Tanzania kwa kuwa inatambua umuhimu wake katika uchumi wa nchi.

Makamu wa Rais ametoa wito kwa IFAD kuona umuhimu wa kuongeza eneo la mradi wa urejelezaji ardhi katika maeneo yanayokabiliwa na ukame Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa Upande wake Makamu wa Rais wa Mfuko huo wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo Dkt. Geraldine Mukeshimana amesema Tanzania imekuwa ni mdau muhimu katika mfuko huo kwa kuwa mchangiaji mzuri na hivyo kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali