MBOLEA AFRIKA BADO TATIZO

0
165

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda amesema mbolea nyingi inayotumika Afrika inatoka nje ya bara hilo, wakati ile inayotengenezwa Afrika inauzwa nje.

Akizungumza mkoani Dar es Salaam kando ya mkutano wa Mifumo ya Chakula Barani Afrika wakati wa majadiliano kuhusu ajenda ya mbolea Barani Afrika na afya ya udongo Pinda amesema, zaidi ya asilimia 90 ya mbolea nchini inaagizwa kutoka nje huku chini ya asilimia kumi ikitengenezwa ndani.

Ameongeza kuwa kwa sasa mbolea inayopatikana nchini inatoka nchi mbalimbali ikiwemo Russia, na kwa sasa upatikanaji wake umekuwa na changamoto kutokana na vita inayoendelea katika nchi hiyo.

Pinda ameongeza kuwa hali hiyo imesababisha bei ya mbolea kupanda na pia mbolea kuadimika na kufikia kuhatarisha usalama wa chakula kwa baadhi ya nchi za Afrika.

Hata hivyo Waziri Mkuu Mstaafu Pinda amesema Serikali za nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania zimeanzisha programu wezeshi za kusaidia upatikanaji wa mbole ili kuleta suluhu ya changamoto hiyo.

Kwa upande mwingine Pinda amesema matumizi ya mbolea yasiyofaa yamechangia kuendelea kuzorota kwa afya ya udongo na kusababisha mavuno kuwa hafifu.