Rais Al-Sisi kuongezewa muda

0
278

Bunge la Misri linatarajia kupiga kura hii leo kufanyia mabadiliko Katiba ya nchi hiyo, mabadiliko yatakayomuwezesha Rais Fattah Al-Sisi kuongezewa muda wa kukaa madarakani hadi mwaka 2030.


Mabadiliko hayo ya Katiba pia yatamuwezesha Rais Al-Sisi kuwa na nguvu zaidi hata kwenye mhimili wa mahakama na kua na uwezo wa kuteua Majaji, jambo ambalo hivi sasa haiwezekani.


Upande unaomuunga mkono Rais Al-Sisi unadai kuwa ni lazima aongezewe muda wa kuongoza Taifa hilo kwa kuwa anahitaji muda zaidi wa kumalizia mageuzi ya kiuchumi ambayo ameyaanza.


Hata hivyo upande wa upinzani nchini Misri unapinga hatua ya Rais Al-Sisi kuongezewa muda wa kukaa madarakani na kusema kuwa Rais huyo amekua akizuia uhuru wa Raia kutoa maoni yao na amekua akituhumiwa kwa kukiuka haki za binadamu.