DED na DC aliyewabagua wananchi kuondolewa

0
210

Rais Samia Suluhu Hassan amesema atamuondoa Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Hanafi Msabaha kutokana na kuwabagua Wananchi katika kupeleka miradi ya maendeleo ambapo mkuu huyo wa wilaya alipeleka mradi mahali ambako haukutakiwa kwenda.

Rais Samia ametangaza uamuzi huo Kibaha mkoani Pwani alipokuwa akifunga mafunzo ya Wakuu wa mikoa na Makatibu Tawala wa mikoa.

“Mkuu wa wilaya anahongwa, mradi anaacha kuupeleka unakotakiwa anaupeleka usikotakiwa, kiasi kwamba Wananchi wanafikia kurudisha kadi za Chama, sisi huku tuna haja kubwa ya mradi mmetuacha mmekwenda kuupeleka kwingine,”

“Mkuu wa Wilaya Hanafi [Hanafi Msabaha] namtimua leo, siwezi kustahimili kadi za chama zinarudishwa, yeye na DED wake, Mkuu wa wilaya yupo, DED yupo kadi za chama zinarudishwa anaulizwa anasema ‘unajua kule wengi Wapinzani’ so what?, sio Watanzania wale,?
hawahitaji kitu?. Amehoji Rais Samia