Rais Ali Bongo awania muhula wa 3

0
245

Wananchi wa Gabon Leo wanapiga kura kumchagua Rais pamoja na Wabunge.

Rais Ali Bongo wa Gabon ambaye aliingia madarakani baada ya Baba yake Omar Bongo aliyekuwa Rais wa Taifa hilo kufariki dunia mwaka 2009, anawania kiti hicho cha Urais kwa muhula wa tatu.

Anakabiliwa na upinzani kutoka kwa wagombea wengine 13 katika kinyang’anyiro hicha cha Urais.

Wagombea wa kiti cha Urais nchini Gabon wanasema wanapambana kuhakikisha Ali Bongo harejei madarakani, ili kuondoa utawala wa familia ya Bongo ambayo imetawala Taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta kwa kipindi kirefu.

Baba yake na Rais Ali Bongo, Omar Bongo alikuwa Rais wa Gabon kwa kipindi cha takribani miaka 42 kuanzia mwaka 1967 hadi mwaka 2009 alipofariki dunia.

Katika chaguzi zote zilizopita matokeo yaliyompa ushindi Ali Bongo yamekuwa yakilamikiwa na wapinzani wake kwa madai ya kuwepo kwa ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi na hata katika uchaguzi huu tayari kumekuwa na malalamiko kadhaa ya ukiukw