Niger yasaini makubaliano ya kijeshi na Mali na Burkina Faso

0
358

Niger imesaini amri inayoruhusu majeshi ya Mali na Burkina Faso kuingia nchini humo kwa ajili ya kuisaidia endapo itavamiwa kijeshi.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya mawaziri wa Mambo ya Nje wa Burkina Faso na Mali kukutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani jijini Niamey.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imetishia kutumia nguvu kumrejesha madarakani Rais Mohamed Bazoum wa Niger aliyepinduliwa na jeshi mwezi uliopita kwa kile kilichoelezwa ni kutokana na hali ngumu ya maisha, mdororo wa uchumi na kuenea kwa ugaidi.

ECOWAS inaendelea kutafuta njia za kidiplomasia kutatua mgogoro huo, laini imetishia kutumia nguvu za kijeshi endapo diplomasia ikishindwa kutoa ufumbuzi.