Pompeo akutana na Guido

0
287

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo amekutana na kiongozi wa upinzani nchini Venezuela na mtu aliyejitangaza kuwa Rais wa serikali ya mpito wa nchi hiyo Juan Guido.

Viongozi hao wamekutana katika nchi jirani ya Colombia huku Pompeo akisema kuwa nchi yake itafanya kila iwezalo kuwasaidia Raia wa Venezuela katika masuala ya kibinadamu na hatimaye kupata serikali itakayowaletea maendeleo.

Pompeo amesema kuwa Marekani itawasaidia Raia wa Venezuela ili kumuwajibisha Rais Nicolas Maduro wa nchi hiyo ambaye amesema kuwa ndio chanzo cha matatizo mengi nchini mwake.