Wanaomuunga mkono Haftar wajisalimisha

0
305

Baadhi ya wapiganaji wanaomuunga mkono Mbabe wa kivita nchini Libya, – Khalifa Haftar wamejisalimisha kwa majeshi ya serikali ya mpito ya nchi hiyo na kuweka chini silaha zao chini.

Wapiganaji hao wamejikuta wakijisalimisha baada ya majeshi ya serikali ya mpito yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa,  kuongeza mashambulio dhidi ya majeshi ya Haftar, ambapo hapo jana ndege yake moja ya kijeshi ilitunguliwa.

Majeshi ya Haftar yamekuwa yakishutumiwa kwa kuhusika na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu kwa kufanya mashambulio yanayowalenga raia na wahudumu wengine wa idara ya afya wanaotoa huduma kwa majeruhi wa mapigano hayo.

Baadhi ya watu katika vitongoji vilivyoko nje ya mji wa Tripoli wamelazimika kuyakimbia makazi yao, baada ya wapiganaji wa Haftar kuendelea kushambulia raia na makazi yao.

Mapigano mapya yalizuka katika mji wa Tripoli baada ya majeshi ya Haftar kuwasili katika mji huo, yakiwa na lengo la kutwaa madaraka na kuanza kupambana na vikosi vya serikali.