Jaji Kazi Mwenyekiti Mpya Zec

0
153

Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Jaji George Kazi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

Aidha Dkt. Mwinyi ametEua wajumbe sita watakaokuwa kwenye jopo hilo la Tume ya Uchaguzi Zanzibar ambao ni Jaji Aziza Idd Suwedi, Idrisa Haji Jecha, Juma Haji Ussi, Halima Mohamed Said, Ayoub Bakar Hamad, na Awadh Ali Said.

Jaji George Joseph Kazi ataapishwa tarehe 28 Agosti, 2023 saa 8 Mchana Ikulu Zanzibar na wajumbe wa Tume hiyo.