Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ameiagiza Menejimenti ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zake kuhakikisha Mipango yote inayopangwa kila mwaka inaendana na mwelekeo wa Viongozi Wakuu wa Nchi, Mipango ya Kitaifa na Kimataifa, Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Kigahe ameyasema hayo wakati akifungua Kikao Kazi cha Menejimenti na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kilichofanyika mkoani Arusha kwa lengo la kujadiliana na kuimarisha ushirikiano katika utatuzi wa changamoto zinazojitokeza wakati wa usimamizi wa kazi zao.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema lengo kuu la Kikao Kazi hicho ni kutafsiri majukumu na shughuli zote za Wizara na Taasisi zake kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika Agosti 19, 2023 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na binafsi zikiwemo taasisi za fedha.