Wanawake wajadili fursa EACOP

0
140

Watanzania wametakiwa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria ili kushiriki vema fursa zilizopo kwenye mradi waBomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP)
kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa jijini Tanga na mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka
EACOP
Catherine Mbatia wakati wa kongamano la Wanawake na manunuzi ya umma na fursa za biashara kwenye mradi huo.

Amesema zipo taratibu zilizowekwa ili kuruhusu kila mtu mwenye sifa ya kushiriki fursa hizo ikiwemo ajira ashiriki bila kipingamizi.

Akizungumza wakati wa kongamano hilo,
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga, Mwanaisha Ulenge amewata Wanawake nchini kushiriki kikamilifu kwenye fursa za kiuchumi zilizopo kwenye mradi huo wa bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki.

Amesema uwepo wa mradi huo ni ukombozi kwa wakazi wa jiji la Tanga na Watanzania wote sababu zipo ajira zaidi ya elfu moja wakati wa ujenzi na baada ya ujenzi.

Kongamano hilo la siku mbili linashirikisha Wanawake zaidi ya 900 kutoka mkoa wa Tanga na mikoa jirani ikiwemo Pwani na Dar es Salaam.