USAID kuboresha matumizi ya Teknolojia

0
142

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi mpya wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID), Craig Hart ofisini kwake jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo yamelenga zaidi kuimarisha ushirikiano katika kuboresha matumizi ya Teknolojia ili kuwezesha huduma nyingine zikiwemo kilimo na afya, ushirikiano katika kukuza taasisi changa, ushirikiano katika kuwezesha miji ya kisasa pamoja na kutumia teknolojia mpya ya 5G katika kuboresha uchumi wa Kidijitali.

Pia ziara hiyo ya Craig Hart ilikuwa ni ya kujitambusha kama Mkurugenzi Mkazi mpya wa USAID nchini Tanzania.