Rais Widodo wa Indonesia atua nchini

0
176

Rais Joko Widodo wa Indonesia amewasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, Rais Widodo amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.Stergomena Tax na maafisa wengine wa Serikali.

Ziara hiyo ya Rais wa Indonesia nchini Tanzania inalenga kuimarisha maeneo mapya ya ushirikiano baina ya nchi hizo ikiwa ni.pamoja na biashara, nishati, afya, kilimo, madini, elimu na uhamiaji.

Akiwa nchini Rais Widodo pamoja na mambo.mengine atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia.Suluhu Hassan Ikulu, Dar es Salaam.

Pia atashuhudia kusainiwa kwa hati kadhaa za makubaliano zinazolenga kuimarisha Diplomasia ya uchumi baina ya Tanzania na Indonesia.