JWTZ: Tunamtafuta aliyesambaza uzushi

0
402

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa
Kuwa kuna habari ya uzushi iliyosambazwa na mandao wa kijami
wa Tanzania Abroad TV (TAT) kwamba Wanajeshi wa ngazi za
juu wa JWTZ wameongezewa mshahara.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa ongezeko hilo limelipwa tarehe 18 Agosti 2023.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaujulisha Umma
kuwa taarifa hivo ni ya uzushi na upotoshaji kwa jamii. Watanzania
waelewe kuwa taarifa hiyo ina nia ovu, hivyo ipuuzwe.

Ukweli ni kwamba hadi leo tarehe 19 Agosti 2023 kwa JWTZ
haijafika tarehe ya kulipwa mshahara. Aidha, hakuna ongezeko
lolote la mshahara au malipo yoyote kwa Wanajeshi wa ngazi yoyote
wa JWTZ valiyofanyika tarehe 18 Agosti 2023 kama ilivyotajwa na
mtandao huo wa kijamii.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaendelea kufuatilia
na kuchunguza kwa kina aliyehusika na upotoshaji ho ili hatua za
kisheria zichukuliwe dhidi yake.