Prof. Assad: Tusiingiliane katika majukumu

0
203

Prof. Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu amesihi bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma kuheshimu nafasi za kila mmoja katika taasisi hizi na kufuata mnyororo wa maamuzi bila kuingilia majukumu ya mwingine ili kuhakikisha utekelezaji mzuri wa majukumu hayo na kupunguzia taasisi za umma hasara.

Aidha, amewataka viongozi wa ngazi za juu kusaidia kukuza uwezo wa wale walio chini yao bila kuona kuwa nafasi zao zitachukuliwa bali kuona kuwa uwezo mkubwa wa watendaji walio chini yao utasaidia kuongeza ufanisi kwenye kazi zao.

Ameyasema hayo akiwasilisha mada katika Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma jijini Arusha.