Balozi Kairuki mrithi wa Migiro London

0
167

Rais Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi Mabalozi watatu na amembadilishia kituo cha kazi Balozi mmoja.

Mabalozi waliopangiwa vituo vya kazi ni Khamis Mussa Omar kuwa Balozi wa Tanzania nchini China kuchukua nafasi ya Balozi Mbelwa Kairuki ambaye amehamishiwa London, Uingereza.

Balozi Ceaser Waitara anakuwa Balozi wa Tanzania nchini Namibia kuchukua nafasi ya Balozi Modestus Kipilimba ambaye amestaafu.

Balozi Dkt. Benard Yohana Kibesse yeye anakuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya kuchukua nafasi ya Balozi John Simbachawene ambaye amehamishiwa Kampala, Uganda.

Balozi aliyehamishwa kituo ni Mbelwa Kairuki ambaye sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Balozi Kairuki anachukua nafasi ya Balozi Asha-Rose Migiro ambaye amemaliza mkataba wake.