Taasisi 248 kufanyiwa mabadiliko ya kimuundo

0
154

Serikali kupitia ofisi ya Msajili wa Hazina imesema itafanya mabadiliko ya kimuundo kwa taasisi 248 zilizo chini ya ofisi hiyo na zile ambazo ina hisa kidogo, ili ziweze kuleta mchango chanya wa kiuchumi kwa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam, Msaliji wa Hazina Nehemia Mchechu amesema ili kufanikisha jambo hilo ofisi yake imeandaa kikao kazi cha siku tatu kitakachofanyika jiijni Arusha ambacho kitahudhuriwa na washiriki kutoka taasisi hizo, lengo likiwa ni kujengeana uwezo wa kuleta ufanisi wa kiutendaji na hatimaye taasisi hizo ziwe na mchango stahiki kwa Taifa.

Amesema katika Kikao kazi hicho kutakuwa na fursa ya kuangalia sheria zinazoongoza taasisi hizo na kuzifanyia marekebisho sheria zitakazoonekana kupitwa na wakati.