Kane atua Bayern Munich

0
184

“Ninafuraha sana kuwa sehemu ya Bayern, moja ya vilabu vikubwa zaidi duniani, na mara zote nimekuwa nikisema nataka kuhama na kuthibitisha uwezo wangu katika kiwango cha juu zaidi katika kazi yangu,” amesema Harry Kane.

Kane amejiunga na mabingwa hao wa Ujerumani kwa mkataba wa hadi Juni 2027, akitokea Tottenham Hotspurs, na atavaa jezi namba 9.

Tangu mwaka 2011, alicheza michezo 435 ya ushindani kwa Spurs na akafunga magoli 280, hivyo kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo.

Kane alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya England katika miaka 2016, 2017, na 2021 na ni mfungaji wa pili kwa kuwa na magoli mengi kwenye historia ya EPL baada ya Alan Shearer.