Rais Samia: Waziri Mkuu simamia mifumo ya Serikali isomane

0
233

Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na taasisi zinazohusika na TEHAMA kuhakikisha mifumo ya Serikali inasomana na kumtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kulisimamia jambo hilo.

Rais Samia ametoa agizo hilo mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkongo wa Baharini wa Airtel-2Africa na huduma ya Intaneti ya 5G.

“Watoa huduma ndani ya Tanzania, benki, wizara ya Elimu, wizara ya Afya na nyingine zote ebu sasa twendeni tukatumie namba moja tu ya Mtanzania, anapoambiwa Samia Suluhu ni namba ishirini ndani ya Tanzania basi taarifa zangu zote, taasisi zote zikivuta namba ishirini awe Samia Suluhu mmoja yule yule,” amesema Rais Samia Suluhu Hassan.

“Sasa hivi naweza nikawa namba ishirini NIDA lakini nikienda benki , shule, afya n.k kuna taarifa zingine hata usalama ndani ya nchi unakuwa na wasiwasi kidogo,” Ameongeza Rais Samia Suluhu Hassan.