Wanamitindo wanne kati ya 200 wa Kitanzania waliojitokeza kwenye usahili wa shindano la Future Face 2023 wamechaguliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye chaguo la awali la shindano la Future Face Duniani kwa mwaka 2023.
Usahili wa kuwapata Wanamitindo hao umefanyika Dar es Salaam na kuratibiwa na Mwanamitindo wa Kimataifa Millen Happiness Magese na kusimamiwa
na Majaji
Millen Happiness Magese mwenyewe,
Ally Rehmtullah, Martin Kadinda na Jamilla Swai.
Wanamitindo hao ni Rachel Juliuu, Joyceller Lasway, Neema Evaresty na Jasinta Makwabe.
Baada ya kupatikana kwa wawakilishi hao, yule atakayechaguliwa kuiwakilisha nchi atakwenda nchini na Nigeria na akifanikiwa kushinda atakwenda Ufaransa au Italia.