Dirisha la udaili chuo cha bandari lafunguliwa

0
172

Wananchi wafurahia huduma zitolewazo na Chuo cha Bandari Dar es Salaam na kupelekea kujitokeza kwa wingi ili kujifunza zaidi kuhusu chuo hicho.

Kufatia maonesho ya nanenane Mkoani Morogoro, wananchi wapata uelewa wa kutosha juu ya mchango wa chuo cha Bandari katika sekta ya uchukuzi. Hivyo kupelekea kufurahia huduma zitolewazo katika chuo hicho wakati wote wa maonesho.

Kwasasa dirisha la udahili liko wazi kwa mwaka mpya wa masomo 2023/2024, ambapo kozi za muda mfupi zimeboreshwa. Mwanafunzi anayejiunga kwa kozi za muda mfupi anatakiwa awe na leseni ya udereva tuu, na kozi hizo zitatolewa kwa muda wa wiki 4 tuu.

Unaweza kutembelea katika website ambayo ni www.bandari.ac.tz pamoja na mitandao ya kijamii ili kupata taarifa mbalimbali za chuo.