Rais Samia azindua Programu ya umwagiliaji ya visima elfu 67

0
145

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua programu ya uchimbaji wa visima elfu 67 kwa ajili ya Wakulima wadogo nchi nzima.

Chini ya programu hiyo mkulima mdogo atachimbiwa kisima na kupewa tenki la maji la lita elfu 5 likiwa limefungwa mtambo wa kutengeneza umeme wa jua pamoja na vifaa vya umwagiliaji vya shamba lenye ukubwa wa heka mbili na nusu.

Programu hiyo itawanufaisha wakulima wadogo ili kuwa na mifumo ya uhakika ya umwagiliaji ambapo kila kisima kimoja kitahudumia wakulima 16, hivyo kuwa na wakulima kumi na sita katika kila kisima kimoja na hatimaye kuwa na hekari Milioni mbili kwa nchi nzima ambazo zitapata maji kwa kutumia programu hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua programu hiyo akiwa mkoani Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale yalipofanyika maonesho na sherehe ya Kimataifa Nanenane.

Programu hiyo ipo chini ya usimamizi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC).