Zanzibar tumekujaaaaa..

0
119

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linaendelea na kongamano la majadiliano kuhusu maudhui yaliyomo kwenye ripoti ya Tume ya Rais ya Haki Jinai.

Baada ya kufanya makongamano kwenye mikoa 5 ya Tanzania Bara, Jumatano hii ni zamu ya Zanzibar.

Kongamano hilo litafanyika katika uwanja wa mpira wa miguu Mwache alale uliopo katika Shehia ya Mwakaje wilaya ya Magharibi A’ Mkoa wa Mjini Magharibi, Jumatano Agosti 09, 2023 kuanzia saa 7:30 mchana.

Litaongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba Chacha na kurushwa Mbashara kupitia TBC1, TBC Taifa na YouTube chaneli ya TBCOnline.