Maonesho Nanenane Mbeya yaongezewa wiki moja

0
124

Rais Samia Suluhu hassan ameongeza wiki moja kwa maonesho na sherehe ya Nanenane kuendelea katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.

“Niunganishe hapahapa ombi la Mheshimiwa Spika kwamba kwa sababu hapo mbele tunakwenda kubomoa eneo hili na kujenga uwanja mzuri utakaokuwa na hadhi ya kimataifa…..
Na nilipofika hapa nikiingia jukwaa lile na moja ya kazi nilizofanya ni kuangalia mchoro na ramani ya uwanja utakavyokuwa,…ni uwanja wa kimataifa haswa sasa kwa sababu kazi hii haitachelewa kuanza naungana na Mheshimiwa Spika kutoa wiki moja zaidi kwa waoneshaji hapa hasa wale waliotoka mikoa ya nyanda za juu kusini ili waweze kuonesha lakini pia polepole kuanza kuchukua vile wanavyohisi vitawafaa kabla shughuli za kubomoa hazijaanza.”

Amesema Rais Samia wakati akizungumza katika kilele cha sherehe hizo za Nanenane na kuongeza kuwa

“Kwa hiyo naungana nawe Mheshimiwa Spika na nimtake Waziri wa Kilimo aruhusu wiki zaidi watu waendelee na shughuli zao hapa.”