RC Homera: Tumetendewa haki

0
107

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema kwa sasa mkoa huo umepata wepesi wa kufanya biashara nje ya nchi kutokana na uwepo wa uwanja wa ndege wa Songwe.

Akizungumza katika kilele cha sherehe na maonesho ya Kimataifa Nanenane mkoani Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale, Homera amesema kwa upande wa safari za anga mkoa huo umetendewa haki.

Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuupatia uwanja huo taa za kuongozea ndege ambazo zimegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 4.7 na zimeboresha mzunguko wa safari za ndege ambapo sasa zipo safari za usiku za saa tatu, nne, tano hadi kunapokucha.

Homera amesema maboresho hayo yamekwenda pamoja na ujenzi wa njia ya kupita ndege ambapo awali ilikuwa chini ya Kilomita mbili na hivi sasa imefika Kilomita 3.3, hivyo ndege kubwa zina uwezo wa kutua katika uwanja huo.