Kibegi cha Simba kimeitangaza Tanzania

0
315

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ataendelea kununua magoli yatakayofungwa na vilabu vya Tanzania kwenye mashindano ya Afrika, ikiwa hamasa ili vifanye vizuri zaidi ya msimu uliopita.

Ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza katika sherehe za Simba Day ambayo ni kilele cha Wiki ya Simba ambapo Rais Samia ndiye alikuwa mgeni rasmi.

Aidha, amesema licha ya utofauti wa vilabu vilivyopo nchini, lakini amevisihi linapokuja suala la mashindano ya kimataifa, kusiwe na uhasama kati yao.

Ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza na kuunga mkono uwekezaji kwenye michezo kwani sekta hiyo inatoa ajira, burudani na kudumisha amani ambapo ametolea mfano ubunifu wa kibegi cha Simba ambao amesema umeitangaza Tanzania na kuunga mkono Royal Tour.

Katika muktadha huo ameisihi sekta binafsi kuwekeza kwenye michezo, akisema mazingira bora ya biashara yaliyowekwa na Serikali yamewezesha biashara kukua, hivyo ni vyema watumie sehemu ya faida yao kukuza michezo.