Wakazi 6, 364 wanufaika na mradi wa maji Inyala

0
114

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim amesema hatua ya
Wananchi kujitolea maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo inapunguza gharama za ujenzi, na fedha ambazo zingetumika kwa ajili ya kununua maeneo zinaelekezwa latika miradi mingine.

Kaim amesema hayo alipokuwa akimpongeza Mwananchi aliyejitolea eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Inyala katika halmashauri ya wilaya ya Geita, mradi unaotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Geita.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA wilaya ya Geita Mhandisi Sande Charles amesema mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha lita elfu 16 za maji kwa saa, unanufaisha wakazi 6, 364.

Mradi huo wa maji wa Inyala ambao nao umezinduliwa na Mwenge wa Uhuru unaoendelea na mbio zake mkoani Geita, umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 463.9 hadi kukamilika kwake.