Rais Mwinyi akutana na Profesa Mkumbo

0
113

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza ushirikiano uliopo na kujifunza zaidi kati ya wizara pamoja na taasisi zake za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo aliyefika Ikulu Zanzibar na ujumbe wake.

Dkt. Mwinyi ameushukuru ujumbe huo kwa utayari wa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mawazo ya kimageuzi yanalolenga kujenga uchumi wa Wananchi wa pande zote mbili katika ushirikiano wa taasisi zinazohusu Mamlaka ya Bandari, Ofisi ya Msajili Hazina, Mamlaka za Uwekezaji pamoja na Tume ya Mipango ya Taifa.