Tumieni fursa ya maonesho ya Nanenane

0
153

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Wananchi kuhakikisha wanatumia fursa ya maonesho ya Sherehe za Wakulima Nanenane kujifunza teknolojia mbalimbali zinazotumika katika shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi.

Ametoa wito huo mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kutembelea maonesho na kukagua mabanda katika Sherehe ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane.

Waziiri Mkuu amewataka Wananchi kufanya uamuzi wa kuingia kwenye kilimo, mifugo na uvuvi huku akisisitiza ni muhimu wajifunze namna ya kufuga wanyama aina zote na kilimo cha aina zote.