Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuweka uwiano wa kutangaza na kuendesha maeneno ya utalii nchini.
Waziri mkuu ametoa agizo hilo alipotembelea banda la TANAPA katika maonesho na sherehe ya Kimataifa ya Wakulima Nanenane mkoani Mbeya.
Amelitaka shirika hilo kutopeleka wageni Serengeti peke yake na badala yake wakumbuke maeneo mengine kama Mikumi ambayo amesema imesahaulika katika siku za hivi karibuni na kuongeza kuwa vilivyopo Serengeti na Mikumi pia vipo.
Waziri Mkuu amesema ni vema kuepuka kukusanya Watalii eneo moja peke yake.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Majaliwa, miundombinu ya usafiri imewekezwa maeneo yote ya vivutio, hivyo utalii ukishamiri itapelekea tija katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Aidha, ameitaka TANAPA kuendelea kuhifadhi, kusimamia na kuyatunza maeneo ya vivutio vya utalii nchini.