Afrika yatakiwa kutumia Diaspora kushauri

0
128

Serikali za nchi za Afrika zimeshauriwa kuwatumia Waafrika wanaoishi nje ya Bara hilo (Diaspora) kushauri namna ambavyo Serikali hizo zinavyoweza kuwekeza katika kuimarisha sekta ya Afya kupitia Ubia na vyuo mbalimbali kutoka Bara la Amerika.

Ushauri huo umetolewa na Profesa Msaidizi kutoka chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya cha Tennessee kilichopo katika jimbo la Tennesee nchini Marekani, Denis Foretia
ambaye ni raia wa Cameroon.

Profesa Foretia amesema hayo
baada ya kupokea ujumbe wa waandishi wa habari kutoka nchi 14 za Afrika ambao ulifika katika chuo hicho kwa lengo la kujifunza maendeleo ya teknolojia na huduma katika sekta ya Afya.

Ameweka wazi kuwa njia pekee ya kuinua sekta ya Afya Afrika ni kupitia Ubia ambapo vyuo vikuu barani humo vitaweza kuwa
na uwezo wa kubadilishana uzoefu na tafiti za afya kupitia Wanafunzi ambao wataweza kuleta mabadiliko kwenye sekta hiyò ya kuanzia teknolojia mpaka huduma zinazotolewa kwa wagonjwa.