Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema mkoa wa Kigoma unakuja kasi sana katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara hivyo viongozi wa mikoa ya Nyanda za Juu kusini wajiangalie.
Bashe ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika sherehe na maonesho ya kimataifa yaliyofanyila mkoa wa Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale.
Bashe amesema “Mheshimiwa Makamu wa Rais nimewaona ndugu zangu hapa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ndugu yangu Homera na makomredi wenzake hapa kwa sababu taifa letu siku zote tukizungumzia Food basket tunazungumzia nyanda za juu kusini.
Lakini nataka tu niwaambie kuna mkoa unakuja kasi kama mkoa wa Kigoma, kwa hiyo wajiangalie, kwa takwimu za mwaka huu Kigoma inakuja haraka sana kwa hiyo tunawaambiwa wamwangalie Kigoma kwa karibu sana.”