Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amevitaja viwanja vitakavyotumika katika maonesho na sherehe ya kimataifa ya Nanenane.
Akizungumza katika ufunguzi rasmi wa sherehe hizo mkoani Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale amevitaja viwanja vitakavyotumika rasmi katika maonesho na sherehe ya kimataiafa ya wakulima Nanenane kuwa ni Kiwanja kilichopo Dodoma na kingine kipo mkoa wa Mbeya ambacho kimetumika katika ufunguzi wa maonesho hayo.
Bashe amesema Rais Samia Suluhu Hassan atazindua mwonekano wa viwanja hivyo ambavyo vitakuwa na hadhi ya kimataifa.
Vilevile amesema miundombinu itaendelea kuwekwa baada ya maonesho hayo na viwanja hivyo vitaendelea kufanya shughuli zake ambazo zitahusika na kilimo,mifugo na uvuzi kwa mwaka mzima na sio tu kuja na kuondoka baada ya sherehe.
Ameongeza kuwa katika viwanja hivyo shughuli za biashara za kilimo zitaendelea na kutakuwa na maeneo kwa ajili ya uchakataji, uzalishaji na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo ndani ya viwanja hivyo hata baada ya sherehe za Nanenane kuisha