Tuzo za taaluma

0
180

Wahitimu 40 wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi – Tanzania (NDC) kilichopo Kunduchi, Dar es Salaam, wametunukiwa shahada na stashahada na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.

Kati yao, wahitimu 33 wamefuzu shahada ya Uzamili ya Usalama na Stratejia huku saba wakifuzu stashahada ya Uzamili ya Usalama na Stratejia.

Katika mahafali hayo ya 11 ya NDC, imeelezwa kuwa chuo hicho kimeshazalisha wahitimu 347 kwa ngazi za juu na wahitimu 688 kwa kozi fupi.