KINANA: CHAMA KITAISHAURI SERIKALI KUHUSU SHERIA YA BODABODA

0
134

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitaishauri Serikali iwasikilize Wananchi inapotaka kutengeneza sheria zinazogusa maisha yao, ili kupunguza migogoro na kero mbalimbali katika jamii.

Akizungumza baada ya kupokelewa wilayani Bariadi, mkoa wa Simiyu, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema, upo umuhimu wa kuangaliwa upya kwa sheria zinazowaumiza Wananchi kama Ile ya usafiri wa bodaboda ambayo kwa sasa inakataza kubeba abiria zaidi ya mmoja.

“CCM inakwenda kuzungumza na Serikali kuiangalia sheria ya usafiri wa pikipiki (bodaboda) ili iruhusu kubeba abiria zaidi ya mmoja,” amesema Kinana.

Hqpo jana akiwa Musoma mkoani Mara, Kinana alieleza kwa kina kuhusu suala la bodaboda kubeba abiria zaidi ya mmoja na wajasiliamali wadogo kunyanyaswa na mamlaka mbalimbali kutokana na sheria zilizopo.

Akifafanua kuhusu usafiri wa bodaboda, Kinana amesema nchi nyingi duniani Wananchi wake wanatumia usafiri huo na kuruhusu kubeba abiria zaidi ya mmoja.