Belligham afungua ukurasa wa magoli

0
288

Kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham amefunga goli lake la kwanza akiwa na timu hiyo na kutangazwa mchezaji bora wa mchezo katika ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Manchester United.

Katika mchezo huo wa kirafiki uliofanyika Houston, Texas, Bellingham alifunga goli dakika ya 6 ya mchezo, ukiwa ni mchezo wake wa pili tangu aliposajiliwa akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani.