Serikali kushughulikia kero za wenye viwanda

0
182

Waziri wa Viwanda na Bashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali itaenda hatua kwa hatua kuhakikisha changamoto wanazopata wenye viwanda zinatatuliwa kwa wakati.

Dkt. Kijaji amesema hayo wakati alipotembelea Kiwanda cha Mbolea ITRACOM, kilichopo Nala mkoani Dodoma kujionea uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho.

Waziri Kijaji amekipongeza Kiwanda hicho kwa utengenezaji wa mbolea usiokua na mchanganyiko wa asilimia 100 ya madini, bali asilimia 50 ni samadi na asilimia 50 ni madini ambao unaleta uhai wa ardhi kwa uasili na ubora wake.

Amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Kiwanda hicho kwa awamu ya kwanza, kitaweza kuzalisha Tani za mbolea millioni 1.2 kwa mwaka huku matumizi ya ndani ya nchi ni Tani 650,000 hivyo hakuna sababu ya kuagiza mbolea nje ya nchi.

Naye Mkurugenzi wa ITRACOM Nduwimana Nazaire ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kutambua juhudi za uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho na ameiomba Wizara ya Viwanda na Baishara kushirikiana na Wizara nyingine katika juhudi za usambazaji wa mbolea hiyo.